El Salvador

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
El Salvador
Ramani ya El Salvador

El Salvador ni nchi ndogo kuliko zote za Amerika ya Kati, lakini yenye msongamano mkubwa zaidi, ikiwa na wakazi 6,290,420 katika km2 21,040.

Imepakana na Guatemala, Honduras na bahari ya Pasifiki.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la nchi kwa Kihispania linamaanisha "Mwokozi" kwa heshima ya Yesu Kristo, ambaye wananchi wengi ni wafuasi wake katika Kanisa Katoliki (47%) au katika madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (33%).

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wananchi wengi ni machotara Wazungu-Waindio (86%) au Wazungu (12%) na wanazungumza Kihispania, ambacho ndicho lugha rasmi na ya kawaida.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu El Salvador kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.